📡 HATARI ZA KUTUMIA WI-FI YA UMMA(Public Wifi) 📶
🦠Kuna shida nyingi zinazotokana na Wi-Fi za umma. Wakati wamiliki wa biashara wanadhani wanawasaidia wateja, ukweli ni kwamba usalama wa mitandao haya ni dhaifu sana au haupo kabisa😐.
💻 Mashambulizi ya Man in the Middle
Moja ya hatari kubwa kwenye mitandao haya ni shambulio la Man in the Middle (MITM). Hapa, Attack hili inafanana na kusikiliza mazungumzo ya siri. Wakati kompyuta inapoingia kwenye Internet, data inatoka A (kompyuta) hadi B (tovuti), lakini hacker anaweza kuingilia kati na "kusoma" mawasiliano hayo. Hivyo, kile ulichofikiri ni siri hakiko tena.
💻 Mitandao Isiyo na Encryption
Encryption inamaanisha ujumbe unaotumwa kati ya kompyuta yako na router ya wireless umeandikwa kwa lugha ya siri, isiyoeleweka na wengine. Mara nyingi, routers zinakuja na encryption ikiwa imezimwa, inahitajika kuwashwa(On) ili Kulinda mtandao.
💻 Usambazaji wa Malware
Kwa sababu ya mapungufu ya programu, wahalifu wanaweza kuingiza malware ndani ya kompyuta yako bila wewe kujua. Mapungufu haya ni kama security bug holes katika Operating system ya App. Hackers wanaweza kutumia hizi kuandika Password ya Kuingilia na kuingiza malware(Virus) kwenye kifaa chako.
💻 Snooping na Sniffing
Wi-Fi snooping na sniffing ni sawa na unavyofikiria. Wahalifu wa mtandaoni wanaweza kununua vifaa maalum na programu kusaidia kusikiliza ishara za Wi-Fi. Njia hii inaweza kuwaruhusu washambuliaji kufikia kila kitu unachofanya mtandaoni — kuanzia kutazama kurasa za wavuti ulizotembelea hadi kudaka taarifa za kuingia kwenye akaunti zako.
💻 Malicious Hotspots
Hizi “rogue access points” zinajaribu kuwadanganya watu kuungana na mtandao wanadhani ni halali kwa sababu jina linaweza kuonekana la kuaminika. Fikira uko katika "Goodnight Inn" na unataka kuungana na Wi-Fi ya hoteli. Unaweza kudhani umechagua sahihi unapobofya “GoodNight Inn,” kumbe siyo. Badala yake, umeunganishwa na hotspot hatari iliyowekwa na wahalifu wa mtandaoni ambao sasa wanaweza kuona taarifa zako za siri.
⚠️Ni Vyema Ukapunguza Matumizi ya WiFi za Bure Za Mitaani.
⚠️Usiripie Au Usijaze Taarifa zako Muhimu Mtandaoni Ukiwa Umeconnect Kifaa Chako na Public WiFi.
📀 Released By @vamelan_tech
JOIN TELEGRAM FOR MORE
JOIN AND WHATS APP CHANNEL FOR MORE